WAKATI ndoa ya staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba’ ikiwa bado haijapoa, msanii mwenzake anayebamba na ngoma kibao ikiwemo Nibebe, Aslay Isihaka ametia neno ndoa hiyo kuwa, kuoa nje ya nchi ni jambo la kawaida tu.
Wiki iliyopita King Kiba alifunga ndoa na mwanamke kutoka Mombasa, Kenya aliyefahamika kwa jina la Amina ambapo ndoa hiyo Aslay ameipongeza na kusema watu wasishangae au kulalamika mtu kuamua kuoa nje ya nchi kwani jambo hilo ni la kawaida tu.
“Kuoa ni jambo la kheri bwana na ni hatua kubwa sana nampongeza sana kaka mkubwa kwani sio jambo la mchezo hilo, lakini watu wanatakiwa kuelewa kuoa nje ya Tanzania ni jambo la kawaida tu kama mtu anavyotoka kwenye kabila lake na kuoa kabila lingine,’’ alisema Aslay.
Post A Comment: