Taarifa zinaeleza kuwa Uongozi wa Arsenal umeanza kufanya mazungumzo ya kimyakimya na Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ili kuchukua nafasi ya Arsene Wenger.
Hatua hiyo imekuja kufuatia Wenger kutangaza kuondoka Arsenal baada ya kuitumikia kwa miaka 22 akiwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo.
Mbali ya Guardiola, Patrick Viera alikuwa anatajwa kuwa moja ya watu wanaopewa nafasi ya kutaka kuinoa Arsenal.
Viera mwenyewe hivi karibuni aliwahi kutangaza angependa kuchukua nafasi ya Wenger japo hakutaka kumwingilia majukumu yake kutokana na heshima aliyonayo kwake.
Jana Wenger alitangaza rasmi kuachana na Arsenal baada ya msimu huu kumalizika baada ya kukaa na kufikiri kuwa amefikia uamuzi sasa wa kuondoka klabuni hapo
Post A Comment: