Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa amesema msichana huyo wananamshikilia na kumhoji kwa kosa la kumdhalilisha kiongozi mstaafu Edward Lowassa na kusababisha taharuki kwa jamii.
“Ni kweli tunamshikilia huyo msichana aliyejitokeza na kudai ni mtoto wa Lowassa hivyo tunamhoji baada ya kukiri amedanganya kwa makosa ya kumdhalilisha na kusababisha taharuki kwa jamii,”amesema Kamanda Mambosasa.
Kamanda Mambosasa amesema wanaendelea na upelelezi na utakapokamilika watamfikisha mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
Aprili 10 msichana huyo alikuwa ni miongoni mwa watu waliojitokeza kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa akitaka kupewa msaada wa kisheria baada ya kudai baba yake ni Edward Lowassa na toka azaliwe hajawahi kumuona baba yake.
Aprili 15 ilionekana video ya msichana huyo ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba radhi kwa kumdhalilisha Lowassa na kusema tukio hilo limechukuliwa kisiasa na sasa anakosa amani.
Post A Comment: