YANGA imeingiza mastaa kadhaa kwenye kikosi kilichopaa alfajiri ya leo Jumapili, kwenda kuivaa Woylata Dicha ya Ethiopia, Jumatano ijayo lakini Ibrahim Ajibu na Vincent Andrew ‘Dante’ hawajasafiri.
Yanga itakuwa chini ya kocha mpya, Noel Mwandila ambaye ni raia wa Zambia anayechukua mikoba ya George Lwandamina aliyetimka kwa madai kwamba ameshindwa kuvumilia jinsi mambo yanavyoendeshwa kienyeji Jangwani.
Mbali ya Ajibu wachezaji wengine ambao watakosekana kwenye msafara wa timu hiyo ni Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Pato Ngonyani lakini wanaongezeka Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa na Kelvin Yondani ambao ni roho ya kikosi cha kwanza cha Yanga.
Yanga ikishinda mchezo huo inafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo italipwa mamilioni ya shilingi hata ikiishia kufungwa mechi zote sita.
Post A Comment: