Kwa kipindi kifupi cha miezi miwili (Januari – Februari 2018) imeripotiwa kuwa watu 334 wamepoteza maisha kutokana na ajali 769 za barabarani.
Hayo yamesemwa leo Aprili 03, 2018 na Waziri wa Mambo ya ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba na kudai kuwa katika kipindi cha 2016 hadi 2018, jumla ya wahanga wa ajali 1,583 walilipwa fidia ya jumla ya Sh7.35 bilioni kutoka kampuni mbalimbali za bima.
Akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu CCM, Rose Tweve ambaye alitaka kujua katika kipindi cha 2016-2018 ni ajali ngapi zilizosababisha vifo na majeruhi.
Mhe. Nchemba amesema katika kipindi cha 2016/18 ajali zimepungua kwa asilimia 43 baada ya kutolewa elimu.
Mwaka 2016 kulikuwa na ajali 9,856 zilizosababisha vifo 3256 na majeruhi 2128. Mwaka 2017 ajali zilikuwa 5310, vifo 2533 na majeruhi walikuwa 5,355.
Post A Comment: