BAADA ya kuishi maisha ya kibachela kwa muda mrefu, rapa mkongwe kwenye gemu la Hip Hop kutoka Marekani, Curtis Jackson III ’50 Cent’ amenasa penzi la mbeba vyuma aitwaye Chanel.
Wawili hao walinaswa juzikati katika pambano la ndondi kati ya Adrian Broner na Jessie Vargas lililofanyika ndani ya Ukumbi wa Barclay’s Arena ambapo wawili hao walionekana wakishikana mikono huku wakiwa katika mapozi ya kimahaba.
Ikumbukwe kuwa, 50 Cent mwenye watoto wawili, alishawahi kuwa katika uhusiano wa muda mrefu kuanzia 2003 na muigizaji Vivica Fox.
Post A Comment: