Zari The Bosslady ameendelea kutupa mawe gizani, na yameendelea kumpata muhusika wake.
Mrembo huyo ametupa dongo lisilopimika kwenye mzani ambalo limeonekana moja kwa moja kumlenga baba watoto wake, Diamond kwa mujibu wa comment za mashabiki ambao wameupitia ujumbe huo.
Zari kupitia mtandao wa Instagram ameweka picha tatu mpya na amendika kwenye moja ya picha hizo ujumbe unaosomeka, “She is also someone’s daughter, treat her how you would want your daughter to be treated by another man. #JustSaying.”
Kutokana na ujumbe huo pia unaonyesha tayari mrembo huyo kwa sasa moyo wake umechukuliwa na mwanaume mwingine ambaye atakuwa amemrithi Diamond kiti chake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: