Serikali imeweka wazi kwamba imebaini njia zinazochangia ongezeko la wahamiaji haramu nchini ambapo imeeleza kuwa baadhi yao husaidiwa na maafisa wa serikali kuingizwa na kusafirishwa kwa njia za zisizohalali hali.
Amesema ongezeko la wahamiaji haramu limepelekea serikali kuweka mitego ya kisasa kuwabaini wahusika wa vitendo hivyo.
Waziri wa Nchemba amesema njia hizo ambazo zimepelekea ongezeko la kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao ni pamoja na kuweka ushiriki wa nchi jirani katika mitego hiyo ambazo ndio njia za wahamiaji hao kupita na kuwachukulia hatua kali za kisheria watendaji wa serikali walioshiriki kutekeleza zoezi hilo ambalo linakiuka sheria za nchi.
Kuhusu vifaa vinavyotumika kuwasafirishia wahamiaji hao haramu Nchemba amesema tayari wametaifisha mali za wahusika hao na kuzimilikisha kwa serikali ili kutoa adhabu kwa wamiliki hao kuogopa kuwapa magari yao watu wasiowaamini na katika kutelekeza hilo serikali haitakua na huruma nao.
Post A Comment: