Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametangaza kanuni mbalimbali za sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
Kanuni hizo ni zile za sheria ya Mawasilinao ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Habari za Mtandaoni) ya mwaka 2018 ijulikanayo kama The Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations, 2018.
Kanuni nyingine ni zile za sheria ya Mawasilinao ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazji katika Redio na Runinga) ya mwaka 2018, ijulikanayo kama The Electronic and Postal Communications (Radio and Television Broadcasting Content) Regulations 2018.
Kanuni hizo ambazo zimetengenezwa chini ya kifungu cha 103 cha sheria ya EPOCA zimesainiwa na Waziri Mwakyembe ambaye ndiye mwenye dhamana ya maudhui ya Habari na Utangazaji.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: