WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika amewataka Jeshi la Polisi kuwa mstari wa mbele katika kukomesha vitendo vya rushwa huku akisisitiza kutekeleza majukumu yao kwa misingi ya utawala bora.

Mkuchika ametoa kauli hiyo jana jioni jijini Dar es Salaam kwa maofisa wa Jeshi la Polisi 32 kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao wamehitimu mafunzo ya Stashahada ya Uzalimi ya Uongozi kutoka Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute).

Mafahali hayo ni ya kwanza kutolewa na taasisi hiyo ambayo wameshirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland na hivyo kufanya mafunzo hayo kutambulika na kukubalika kimataifa kuhusu masuala ya uongozi.Hivyo akizungumza na maofisa hao pamoja na wageni wengine waalikwa ,Mkuchika amewapongeza wahitimu hao lakini awakata kuwa mstari wa mbele wao pamoja na jeshi la polisi kwa ujumla wake kupambana na komesha rushwa.

Amesema katika mataifa mbalimbali maeneo ambayo rushwa inaangaliwa sana ni katika Mahakama na Polisi .Hivyo ni vema polisi nchini wakawa mstari wa mbele kukomesha rushwa.

"Mataifa mengi yanapimwa katika mambo ya kupambana na rushwa pamoja na kuangalia maeneo mengine pia wanaangalia na Jeshi la Polisi.Na kwa bahati mbaya kwenye nchi nyingi baadhi ya polisi wamekuwa wakituhimiwa kujihusisha na rushwa, hivyo ni vema waliopata mafunzo hayo ya uongozi wakawa mabalozi wa kukemea rushwa nchini,"amesema Mkuchika

Share To:

msumbanews

Post A Comment: