Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 7 kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe kufanya Operesheni ya kuwaondoa wavamizi wa nchi jirani wanaodaiwa kulima na kufiga ndani kisiwa cha Izinga kilichopo ndani ya Pori la Akiba la Kimisi mkoani Kagera.
Ametoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake wilayani Karagwe mkoa wa Kagera muda mfupi baada ya kupokea taarifa na malalamiko ya kukamatwa kwa mifugo ya Watanzania ndani ya kisiwa cha Mubali huku kukiwepo mazao yanayodaiwa kulimwa na wananchi wa Rwanda katika kisiwa kingine cha Izinga.
“Ndani ya siku saba hicho kisiwa cha Zinga msafishe kila kitu, Mkuu wa Wilaya msaidie mtengeneze kikosi kiende kule kitoe takataka zote zilizoko kule, inakua ngumu kuadministrate (kutawala) wengine wa kwetu tunawatoa alafu wa nchi nyingine wamekaa, unatawalaje?”. Aliuliza kwa mshangao Dk. Kigwangalla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Lut. Col. Michael Mutenjele (kushoto) wakati wakivuka kivuko cha Ruvuvu wakati wa ziara yake ya kutembelea na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana
Post A Comment: