Jeshi la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watu 14 kwa tuhuma za mauaji, wizi pamoja na kukutwa na noti bandia
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa watuhumiwa 10 kati ya hao wanaoshikiliwa wanatuhumiwa kwa kosa la mauaji, watatu kwa tuhuma za wizi na mmoja kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia.
Kwa mujibu wa Kamanda Mtafungwa amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako ulifanyika katika wilaya mbalimbali za mkoa huo na kubaini watuhumiwa hao wakiwemo 10 waliotekeleza mauaji kwa imani za kishirikina.
Msikilize hapa chini Kamanda Wilbroad Mutafungwa akifafanua zaidi
Post A Comment: