Jumla ya watu 308 wameripotiwa kuugua Kimeta kuanzia  Januari mwaka 2017 hadi kufikia Desemba mwaka jana mkoani Arusha.
Katibu tawala mkoa wa Arusha, Richard Kwitega, ametoa taarifa hiyo leo Machi 15  katika Kikao cha Kamati ya UshauriM(RCC) ya mkoa wa Arusha na kueleza kuwa hadi sasa bado kuna watu wameendelea kuugua ugonjwa huo.
Kwitega amesema ugonjwa wa Kimeta umekuwa ukitokea na kwa kujirudiarudia mkoani Arusha, na kwamba Novemba  mwaka juzi ugonjwa huo ulianza kuripotiwa wilayani Monduli .
"Ugonjwa huu ulitokea katika kata ya Selelana kusababisha vifo vya wanyamapori pamoja na mifugo na kuleta madhara kwa baadhi ya watu," amesema
Hata hivyo, amesema  kuna jitihada zinaendelea katika kupambana na ugonjwa wa kimeta.
Amesema  Mkoa wa Arusha unay timu ya afya moja (one Health Team) ambayo inajumuisha wataalamu wa mifugo na afya kwa kuzishirikisha wilaya katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo.
"Jitihada zimekuwa zikikabiliwa na changamoto za ufinyu wa bajeti kwa ajili ya mafuta, posho na vifaa hivyo kukwamisha utekelezaji kwa maana ya mafunzo, tiba na chanjo na ufatiliaji wa kina katika jamii," amesema.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya wakazi wa Arusha, Joram Lazier na Edna Joseph, wameiomba, Serikali kuongeza kutoa elimu juu ya ugonjwa wa kimeta ili kukinga wasiugue.
"Huu ni ugonjwa unatoka kwenye mifugo kwenda kwa binaadamu hivyo, tunaomba tu elimu zaidi,"amesema
Kwa upande wake Joseph amesema  bado wananchi wengi hasa wa vijijini hawajuwi dalili za ugonjwa huo na hatua za kuchukuwa mara baada ya kuugua.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: