Baadhi
ya Waratibu wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za
Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakifuatilia majadiliano kwenye mkutano huo
Jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Demokrasia na Utawala Bora-
ICGLR, Balozi Ambeyi Ligabo akifuatiwa na Mwenyekiti wa Mkutano, Service
Julie kutoka Congo.
Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakifuatilia majadiliano
Mwenyekiti wa mkutano, Service Julie kutoka Congo (wa pili kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR.
Washiriki kutoka Tanzania wakifuatilia majadiliano kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma akimwakilisha Kamishna wa Madini, Prof. Shukran Manya na Mhandisi Fadhili Kitivai (kutoka Wizara ya Madini).

Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano Jijini Arusha.
Wataalam
wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR
wamekutana Jijini Arusha ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu
madini hayo kwa maslahi mapana ya nchi hizo.
Mkutano huo wa
siku mbili ulifunguliwa juzi Machi 27, 2018 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo ambapo alisisitiza kuwa Nchi Wanachama wa ICGLR wanao
wajibu wa pamoja kuhakikisha malengo waliyojiwekea yanafikiwa kwa
manufaa ya wanachama wote.
Gambo
alizungumzia changamoto mbalimbali zinazozikabili Nchi Wanachama ambazo
ni uvunaji haramu wa madini, utoroshwaji wa madini, uharibifu wa
mazingira, ukosefu wa teknolojia na baadhi ya Nchi kuwa na changamoto za
Kiusalama.
Hata hivyo
alisema changamoto hizo zisiwe sababu ya kurudi nyuma badala yake juhudi
za pamoja, mshikamano wa dhati unahitajika ili kukabiliana na
changamoto hizo na kuhakikisha ufumbuzi unapatikana kwa maslahi mapana
ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Nchi Wanachama
ni Tanzania, Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo
(Kinshasa), Congo (Brazzaville), Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan
Kaskazini, Uganda na Zambia.
Tanzania
imekuwa Mwanachama rasmi wa ICGLR Mwaka 2008 na tangu wakati huo
imeendelea kutekeleza malengo ya mpango wa ICGLR ili kufanikisha
udhibiti wa uvunaji haramu wa madini na kuhakikisha manufaa ya pamoja ya
rasilimali husika yanapatikana.
Post A Comment: