Msanii wa Filamu Bongo, Wastara amedai alipokuwa akichangisha michango ya matibabu yake ya awali msanii Diamond alishindwa kumsaidia kutokana na mtu aliyemwagiza kwake kumuhisi ni mwizi.
Muigizaji huyo ameiambia Kikaangoni, EATV kuwa licha ya kuwasiliana na meneja wa Diamond, Babu Tale na kumueleza kuwa kijana huyo kamwaagiza yeye bado hakupata msaada wowote.
“Mtu akaanza kumtafuta Diamond, akamwaambia njoo ofisini, kufika akaambiwa mara njoo nyumbani, akakaa hadi saa tisa za usiku hakumpata Diamond, mwisho akaanzwa kutafutwa yule kijana na watu wake Diamond akionekana yule mtoto mwizi, kwa hiyo kwa Diamond tukawa tumefeli,” amesema Wastara.
“Kutoka kwa Diamond tukaenda kwa Alikiba, nikamueleza akaniambia sawa nitakusaidia kuna watu wanataka show Mombasa lakini hela yao ndogo ila kwa kuwa una shida nitaenda nikirudi nitakupa hela,” ameeleza.
Ameongeza kuwa mwisho wa siku michango aliyoipata ni kutoka kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Hassan Suluhu, Alikiba pamoja na mbuge ambaye hakumtaja jina, hao ndio waliowezesha matibabu yake ya awali ambao kufanyiwa operesheni ilishindikana.
Post A Comment: