Mauaji ya wanawake yanayoambatana na imani za kishirikina yameibuka upya Mkoani Shinyanga na kuwatia hofu wakazi wa Songambele kata ya Salawe Wilayani Shinyanga na kuwafanya wananchi washindwe kufanya shughuli zao za kimaendeleo.
Wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa wanahisi mwanamke mmoja huuawa kila wiki kuanzia mwezi Disemba mwaka jana (2017) kwa kukatwa mapanga au kunyongwa na watu wasiofahamika ambapo hutoweka na viungo vya siri vya wanawake wanaouawa.
Wakizungumza mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Shinyanga inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Josephine Mtiro na kusema kuwa hali hiyo inawatia wasiwasi kuendelea kuishi kijijini hapo.
Kwa habari kamili sikiliza hapa chini
Post A Comment: