Zoezi la Uokoaji na upelekaji wa Misaada katika Vijiji vya Sinya na Leremeta Vilivyopo Wilayani Longido Mkoani Arusha vilivyozingirwa na maji kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani humo,limeendelea baada ya kupokea Mitumbwi miwili kutoka katika shirika la Honeyguide Foundation  itakayosaidia kuvusha Vyakula pamoja na watu wenye mahitaji maalum.

Wakipokea mitumbwi hiyo,wananchi wa Vijiji hivyo Mwananchi Solomon Lazer amesema kuwa mitumbwi hiyo itakuwa msaada kwao nakuiomba serikali kuongeza nguvu,huku mmoja wa wafanyakazi wa Shirika lilitoa msaada huo akisema Zoezi la uokoaji linakwenda vizuri nakusema endapo mvua zitaendelea kunyesha kuna haja ya kupatiwa vifaa vya kisasa zaidi.


Kwa upande wake Afisa tawala wa Wilaya hii Thoba Nguvila ambaye ni makamu mwenyekiti wa kamati ya maafa anasema mpaka sasa hawajapokea taarifa ya Vifo iliyosababishwa na mafuriko hayo.

Mbunge wa Jimbo hili Dokta Steven Kiruswa akiwashukuru wadau wanaoendelea kutoa msaada nakuwashauri wananchi hao kuhama endapo hali itazidi kuwa mbaya.

Mafuriko hayo yamesababishwa na Mvua zinanoendelea kunyesha Wilayani humo,huku kaya zaidi ya Mia tatu zikizingirwa na Maji na kusababisha kukosa baadhi ya huduma muhimu nakukosekana kwa mawasiliano.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: