Shirikisho la Riadha nchini (RT) kupitia kwa Katibu wake mkuu Wilhelm Gidabuday, limekiri baadhi ya wadhamini kujitoa katika kipindi hiki ambacho timu ya taifa ya riadha inajiandaa na mashindano ya Jumuiya ya Madola.
Gidabuday amesema kambi ya timu hiyo imekuwa na mafanikio japo bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa fedha za kutosha kupata kila kitu wanachohitaji.
''Baadhi ya wadhamini wametukimbia na wamesimamisha udhamini wao kwenye vitu ambavyo RT haiwezi kutatua sababu kubwa ni kutokuwepo kwa baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa akiwemo Alphonce Simbu'', amesema .
Kwa upande mwingine wachezaji sita wanaounda timu ya taifa ya riadha wamesema watafanya vizuri kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kuanza Aprili 04 hadi 15 mwaka huu katika jiji la Gold Coast nchini Australia.
Post A Comment: