Baadhi ya wananchi wa kata ya Bugogwa katika Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza wamelalamikia kutopewa elimu na viongozi wanaondesha zoezi la uandikisha fomu za uombaji uraia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema kuwa wengi wao wanapata shida pale wajazapo fomu kutokana na kutokujua kusoma na kuandika, kwani imewaletea usumbufu kufikia hatua ya kusitisha shughuli zao kwa muda ili washughulikie ujazaji fomu hizo.

"Unakuta mtu anaishi mbali na kituo, na nyumbani hana mtu wa kumsadia kujaza fomu na utaratibu wa kufuata baada ya kujaza, inafikia hatua zoezi hilo linafanyika saa 12 asubuhi mpaka jioni bila mafanikio, alisema mwananchi aliyetambulika kwa jina moja la Makoye.

Bi.Suzana ambaye anasema anatembea umbali mrefu kufika kituoni hapo bado anakutana na foleni kubwa lakini aliporuhusiwa kuingia katika chumba cha kupigia picha (passport size) kwa ajili ya kujaza fomu hizo aliambiwa nguo aliyovaa hairuhusiwi kupiga nayo picha akarudi nyumbani bila mafanikio, mpaka leo yupo kituoni kwa ajili ya upigaji picha.

"Kipindi tunafuata fomu za uombaji uraia hatukuambia hatukupewa utaratibu kuhusu uvaaji wa mavazi yenye rangi inayostahili na ipi isiyostahili tunafika kupiga picha ndo wanatueleza nguo hazifai kupiga nazo picha na pale wapo watu wa aina wengi huwezi kuazima nguo kwa muda huo kwani maradhi ni mengi, ukiangalia ninapotoka ni mbali na kituo kilipo tunapata shida sana", alisema Bi. Suzana.

Hayo yamejiri kufuatia Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuanzisha zoezi la kuandikisha, kusajili na kuwatambua wananchi wa kuwapa Vitambulisho vya Taifa  ikilenga kutoa vitambulisho hivyo kwa Watanzania wote wanaostahili ifikapo Desemba 2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: