Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Michael Wambura ameeleza suala Kamati ya Maadili ya shirikisho ni la kimkakati zaidi na si la kisheria.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam Wambura amesema suala hilo lilianza miaka 14 iliyopita akiwa raia wa kawaida tuu.Wambura anatuhumiwa kufoji barua na kupokea malipo yasiyo halali kutoka Kampuni ya JICK System Ltd,pia kushusha hadhi ya TFF.
Akizungumzia zaidi suala hilo Wambura ameeleza tatizo lililopo ni uenyekiti wa TFF, fedha na ajira za TFF hasa nafasi ya Katibu Mkuu.Pia Wambura amesema kuwa kama Makamu Mwenyekiti wa TFF ataendelea kufanya kazi kama kawaida na lawama hizo zishindwe kabisa.
Ameongeza, kuwa kuna tatizo kubwa sana ndani ya Shirikisho hilo na wananchi watalijua mapema na ameitaka kamati tendaji kufikiri tena kabla ya kufanya maamuzi.Hata hivyo amesema anasubiri barua rasmi ya kamati hiyo na ndipo atakuwa na cha kuzungumza,hivyo anasubiri maana kwa sasa amesikia tu taarifa kuhusu kusimamishwa kujihusisha na soka.
Kwa upande wa Wakili wa Wambura Emmanuel Muga amesema, kikao hakikufuata sheria hali iliyompelekea kushindwa kufanya kazi yake, amesema barua ya mwito ilicheleweshwa na ilipelekwa nyumbani kwake ili hali Wambura yupo TFF.
Pia ameeleza kanuni ya 48 ya maadili ya TFF inayoeleza kuna siku 3 za kuitikia mwito haikuzingatiwa na pia kamati haikuzingatia kanuni ya 58 inayoeleza kuhusu kesi na kupanga siku ya kuleta vielelezo na mashahidi haikuzingatiwa kwa mteja wake.
Pia Muga ameeleza kuwa kikao hicho hakikutoa majibu ya moja kwa moja na walieleza watatoa uamuzi siku nyingine.
Post A Comment: