.
Mkazi wa Salasala na Diwani wa Kata ya Magomeni, Dk.Julian Bujugo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na ubomoaji wa nyumba zao ambapo ni kinyume cha sheria jijini Dar es Salaam.
WAKAZI wa Kata tano wa Jiji la Dar es Salaam wamemuomba Rais Dk. John Magufuli kuingilia kati ubomoaji wa nyumba kata hizo katika kupisha ujenzi wa bomba la Maji la Ruvu.
Kata zitazoathirika kwa makazi katika upanuzi wa ujenzi wa bomba la Ruvu Juu ni Wazo, Salasala, Bunju Mbweni pamoja na Mabwepande
Akizungumza na waandishi wa habari mkazi wa Salasala Dk. Julian Bujugo amesema hawapati usingizi tangu walivyoambiwa wavunje nyumba zao wakati sheria inawalinda.
Amesema sheria ya mwaka 2001 ya Dawasa katika ujenzi wa mabomba yao ni mita tano (5) lakini sasa wameambiwa ni mita 15 ambazo hiziko katika sheria
Bujugo amesema kuwa katika suala hilo walitaka kwenda mahakamani lakini waliona wazungumze ili kuweza kusema kwa Serikali kitu ambacho kinawatatanisha kuhusu uboaji huo.
Amesema kuwa Rais Dk.Magufuli ni mtetezi wa wanyonge,hivyo kwa wakazi wa kata tano jicho lao ni kwa Rais na sheria inawafanya kuwa halali.
Bujugo amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuangalia suala lao kwani hawana sehemu ya kukimbilia
Post A Comment: