Wachimbaji wa madini waombwa kusaidia kupunguza tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike kwa kusaidia shughuli za maendeleo ya ujenzi wa hostel za wasichana katika shule za sekondari nchini.
Hayo yamesemwa na katibu wa mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Ester Yona wakati akipokea mabati 360 yaliyotolewa na mgodi wa Shanta tawi la singida kusaidia jitihada za mbunge wa jimbo hilo Dr Mwigulu Nchemba ambaye ameanzisha ujenzi wa hostel za wasichana katika kila shule ya sekondari jimboni kwake.
Bi Ester amesema kwasasa tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike bado lipo katika jimbo hilo na wengi wanaacha masomo na wengine hawana ufaulu mzuri katika masomo yao jambo lilopelekea mbunge wa jimbo akishirikiana na madiwani na wananchi kuanza ujenzi huo kusaidia kupunguza tatizo hilo na kutengeneza wanawake wasomi ambao watalisaidia taifa baadae katika nyanja mbalimbali.
Ameongeza kusema kuwa msaada waliopata wa bati 360 watapelekea katika majengo ambayo yapo teyari kwa kupauliwa yaliyopo katika kata ya kyengege na kata ya Ntwike ambapo wamepanga ifikapo mwezi mei mwaka huu yaanze kutumika.
Naye meneja mkuu wa Singida Shanta mining mhandisi Filbert Rweyemamu amesema wameamua kusaida mabati hayo kwa ajili ya ujenzi wa hostel inatokana na sera za serikali katika uajili wakina mama wapewa kipaumbele unakuta kuna kasoro kwasababu wale unawaitaji wenye sifa za kutosha uoande wakina mama hawapatika hivyo walivyosikia wazo la mbunge kuwapa kipaumbele wakina mama kupata elimu wameamua kumuunga mkono kuchangia vifaa hivyo vyenye thamani ya milioni Tisa.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba lino Mwagale amesema anawashukuru Shanta kwa kusaidia kumuunga mkono mbunge Dr Mwigulu ambaye ameamua kuwekeza katika elimu, sekta ya afya na maji, ujenzi wa hostel utasaidia kuongeza mahudhulio ya wanafunzi wa kike mashuleni na hata umalizaji wao utaongezeka zaidi na kupata wataalam wakubwa kutoka halmashauri ya iramba.
Halmshauri ya wilaya iramba inachangamoto ya wanafunzi wa kike kushindwa kumaliza mashomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mbali kutoka sehemu za makazi na shule ambao wanapita katika mito na mvua zikinyesha wanakwama kwenda na tatizo kubwa ni mimba na kwa mwezi ulioisha mwanafunzi mmoja amebainika kuwa na mimba na hatua za kisheria zinaendelea kwa akiyehusika.
Post A Comment: