Wabunge sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepata ajali ya gari wakitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilitokea jana usiku majira ya saa tatu mkoani Morogoro ambapo majeruhi walikimbizwa hospitali ya mkoa huo.
Hata hivyo wabunge hao leo asubuhi wamepatiwa rufaa kwa ajili ya kwenda kutibiwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili na kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Wabunge waliopata ajali wanatokea visiwani Zanzibar, wabunge hao ni pamoja na Haji Ameir Haji, Khamis Ali Vuai, Bhagwanji Maganlakal Meisuia, Makame Mashaka Foum, Juma Othman Hija.
Post A Comment: