UONGOZI wa Simba, umedai kuwa hauwezi kumuuza mchezaji wao Mganda, Emmanuel Okwi kwa timu ya Al Masry na umesisitiza kuwa sasa wa­nawaza kuhusu ubingwa na siyo kuuza wachezaji.

Okwi ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea timu ya Sports Club Villa ya kwao Uganda kwa ada ya shilingi milioni 115, ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa nayo 16 akifuatiwa na Obrey Chirwa mwenye 12.

Katika mechi mbili za Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry, ilielezwa kuwa Waarabu walivutiwa na ‘udambwi­udambwi’ wa Mganda huyo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Simba, Said Tully, alisema kuwa kwa sasa wanachoweza kuwaza ni kuhusu mechi zao kumi zilizobakia kwenye ligi kuu, masuala ya kuuza wachezaji bado muda wake, ila kuhusu taarifa za kutakiwa na Al Masry hawajaweza kuzungumza nao suala hilo.

“Tumebakiwa na me­chi kumi hivyo mipango yetu na mikakati yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zote na kuweza kuchukua ubingwa lakini pamoja na ushindani wa kwenye ligi tunajua kuwa kuna makosa nyuma timu imefanya na kuweza kushindwa kupata pointi lakini sisi kama uongozi tumeji­panga kuhakikisha kuwa makosa hayo hayajirudii na hakuna njia ny­ingine zaidi ya kufanya maandalizi ya kutosha na kuweza kushinda mechi zote.

“Hakuna maongezi yoyote tuliyofanya na Al Masry kuhusu kumuuza Okwi na huu siyo muda wa kuuza wachezaji na agenda yetu namba moja sasa hivi ni kush­inda ligi na kuchukua ubingwa na hatuwezi kuzungumza masuala yoyote, hivyo tutazung­umza hilo msimu ukiwa ushamalizika, sasa hivi agenda yetu ni kupam­bana kama tukiweza kuchukua ubingwa au tukishindwa ndiyo tut­ajua nani tumuuze nani tubaki naye,” alisema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: