WAKAZI
wa Jiji la Dar es Salaam kupitia Umoja wa Rudisha uzalendo Tanzania
(RUTA) umepongeza juhudi za Rais Dk.John Magufuli na watendaji kazi wake
katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini huku wakitangaza kufanya
maandamano ya amani Aprili 12 mwaka huu.
Hayo
yameelezwa jana na Mratibu wa umoja huo Charles Masele jijini Dar es
Salaam ambapo alisema kuwa wananchi wengi wamevutiwa na wanaunga mkono
juhudi za Rais Magufuli, hivyo katika kumpongeza wameandaa maandamano ya
amani yatayohusisha watu wa itikadi zote yatakayofanyika Aprili 12
mwaka huu kuanzia Karume hadi viwanja vya Mnazi mmoja kuanzia saa moja
hadi saa tano asubuhi .
Wakizungumza
zaidi wadau hao walisema hawana budi kuunga mkono juhudi za Rais kwani
huduma nyingi zimeboreshwa zikiwemo miundombinu, afya hasa kwa akina
mama na elimu ambayo hutolewa bure, pia mikopo ya elimu ya juu ambayo
hutolewa kwa wanafunzi wa hali ya chini.
Aidha
wameeleza utiifu wa Rais na watendaji wake wa serikali na taasisi
binafsi kwa namna wanavyothamini na kuhudumu kwa haki na usawa hivyo
wameona ni vyema kumuunga mkono na kumuombea.
Pia
umoja huo umewataka vijana na watu wa kada mbalimbali kuunga mkono
juhudi hizo kwani zinafanywa kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na
baadaye.
Post A Comment: