Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF leo limetangaza kumteua Ammy Ninje kuwa kocha wa muda wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 NgorongoroHeroes.

Ngorongoro Heroes inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco na Msumbuji, kabla ya kuwavaa DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana (AFCON U20).

Kocha huyo ambaye amewahi kukaa kwenye benchi la ufundi la klabu ya Hull City ya nchini England, sio mara ya kwanza kufundisha timu ya taifa ambapo mara ya kwanza aliiongoza Kilimanjaro Stars kwenye michuano ya kombe la CECAFA japo haikufanya vizuri.

Timu hiyo inaundwa na baadhi ya nyota waliofanya vizuri kwenye kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za AFCON U17 mwaka jana nchini Gabon.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: