Katibu Mtendaji wa TAVITA, Otieno Peter,(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Kutoka kushoto ni Mweka hazina wa TAVITA, Norbert Kobwino, Otieno Peter na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Shabani Amiri.
Mkutano huo ukiendelea na waandishi wa habari. 

TASWIRA ya Vijana Tanzania (TAVITA) imelaani vikali taarifa za uchochezi zinazofanywa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vingine,  kitendo kinachoweza kupelekea kuligawa taifa.

Hayo yemeelezwa na Katibu Mtendaji wa TAVITA, Otieno Peter, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kwamba kila mwananchi ana fursa ya kulitumikia taifa ili kuchochea maendeleo badala ya kuchochea uvunjifu wa amani.

Aidha amewaomba viongozi wa dini na asasi za kiraia kuelimisha jamii juu ya madhara yanayoweza kujitokeza ikiwa nchi  ikiingia kwenye machafuko.

TAVITA imepongeza serikali ya Rais John Magufuli namna ambavyo imeweza kufanya mambo makubwa hasa kwa kipindi kifupi na hivyo Watanzania wanapaswa kuiunga mkono.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: