MSHAMBULIAJI wa Yanga Amissi Tambwe raia wa Burundi atalazimika kukaa nje wiki mbili kutokana na upasuaji mdogo aliofanyiwa mwanzoni mwa wiki hii kutokana na majeraha ya goti yaliyokuwa yakimkabili.


Tambwe alipatwa na majeruhi ya goti katika mzunguko wa kwanza ambapo amecheza mechi chache za ligi kutokana na kujitonesha mara kwa mara.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh ameiambia Spoti Xtra kuwa, Tambwe atalazimika kukaa nje wiki mbili kujiangalizia hali yake baada ya upasuaji huo kabla ya kurejea kikosini kuanza mazoezi na timu hiyo.

Hiyo inamaanisha kwamba mechi zote mbili za kimataifa dhidi ya Township atazikosa na hata za ligi dhidi ya Mtibwa, Kagera na Stand nazo ataziangalizia jukwaani kama mwanachama wa kawaida, Mzee Akilimali.

“Tambwe amefanyiwa upasuaji mdogo, hivyo hatakuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza mchezo huo kutokana na majeraha yake hayo, anatakiwa akae nje wiki mbili ndio aanze mazoezi mepesi,” alisema Hafidh. Waliokuwa majeruhi ni Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Juma Mahadhi ambaye alikuwa akisumbuliwa na homa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: