Rapa Stamina ambaye kwa pamoja na Roma Mkatoliki anaunda kundi la ROSTAM amefunguka kuonyesha kushangazwa na maamuzi yaliyofanywa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza kumfungia Roma Mkatoliki
Stamina amefunguka hayo baada ya kusikia Roma Mkatoliki amefungiwa kujihusisha na sanaa kisa kutofanya marekebisho ya wimbo wao wa Kibamia na kusema kuwa awali walipoongea na Waziri huyo aliwapa miezi sita ya kufanya marekebisho ya wimbo huo sasa iweje amechukua maamuzi ili hali hata muda ambao walipewa haujakwisha. 
"Kibamia ilitoka Novemba 22, 2017 na BASATA Roma Mkatoliki tuliitwa Disemba 6, 2017 na Mhe. Waziri akasema wametupa miezi sita na leo ndio kwanza Machi 1, 2018 mbona miezi sita bado au miezi sita ya Tanzania iko tofauti na kalenda ya dunia nzima? Mna tatizo gani na wasanii wetu BASATA na Wizara? Mnakuza au mnauwa sanaa? alihoji Stamina 
Stamina na Roma Mkatoliki kwa pamoja wanaunda kundi la ROSTAM ambao ndio wamiliki wa wimbo huo wa Kibamia lakini matokeo yake Roma Mkatoliki amechukuliwa adhabu peke yake kwa wimbo wa kundi hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: