Kikosi cha timu ya Simba kimelazimishwa sare ya bao 3 – 3 dhidi ya timu ya Stand United mchezo wa ligi kuu soka Tanzania uliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waliyo funga mabao kwa upande wa kikosi cha Simba ni Asante Kwasi, Nicolas Gyan na Laudit Mavugo wakati kwa upande wa Stand United wakiwa ni Aron Lulambo, Nicolas Gyan na Bigirimana Blaisa.
Kwa matokeo hayo Simba sasa inaongoza ligi kwa jumla ya pointi 46 dhidi ya  Yanga SC wenye pointi 40 wakati nafasi ya tatu ikishikwa na Azam FC wenye 35.
Matokeo hayo yana kuwa na manufaa makubwa kwa Stand United ambao sasa wanafikisha alama 21na kupanda hadi nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: