Kikosi cha simba kimeanza safari ya kurejea nyumbani Tanzania, baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry kuchezwa jana.

Simba wameanza safari hiyo dakika kadhaa zilizopita kuelekea Mji Mkuu wa Misri, Cairo, kisha watapanda ndege rasmi kwa safari ya Tanzania.

Safari hiyo imeanza baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, kufuatia suluhu ya 0-0 jana Jumamosi .

Al Masry walifanikiwa kusonga mbele mpaka hatua ya makundi, kutokana na faida ya bao la ugenini ambapo katika mchezo wa kwanza uliopigwa Tanzania, timu hizo zilienda sare ya 2-2.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: