Sehemu ya kunyweshea mifugo iliyojengwa katika ​​Soko la Kimkakati la Longido,  Wilayani Longido kwa ufadhili wa  Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Baadhi ya mifugo wakiwa katika eneo la kunywa maji kablaya kuuzwa katika Soko la Kimkakati la Longido,  Wilayani Longido ambalo limejengwa kwa  ufadhili wa  Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Serikali kupitia, Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), imetekeleza maombi 5 ambayo yanawasaidia wafugaji hao  kuongeza thamani ya mifugo yao  kupitia Soko la Kimkakati la mifugo Longido lililojengwa na Program hiyo.

Mwishoni mwa mwaka 2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira ,Kazi,  Vijana na Watu wenye Ulemavu ) Mhe.Jenista Mhagama, alikuwa na ziara ya kukagua  ujenzi wa soko hilo wilayani humo, ambapo  baada ya ukaguzi alikutana na wafanyabiashara ya mifugo, ambao  waliwasilisha maombi  5,  ambayo yangeweza kuongeza Thamani Biashara za Mifugo na kutatua  kero zote  za wafanyabiashara wa mifugo wilayani humo.

“Serikali ya awamu ya tano imeamua kuwasikiliza watu wanyonge na ambao wanajituma kuchapa kazi, lakini pia lengo la Program ya MIVARF ni kuongeza kipato kwa  wananchi hasa waishio vijijini, kwa mantiki hiyo nilimuelekeza Mratibu wa Program Kutekeleza maombi yao haraka sana ili wafugaji hawa wapate tija ya ufugaji kupitia soko hili” alisema Mhagama

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Mifugo wilayani Longido, Saruni Laizer amesema maombi waliyowasilisha serikalini ili waweze kupata tija ya mifugo kupitia soko la Kimkakati la Mifugo Longido yamefanyiwa kazi na Program ya MIVARF ndani ya miezi mitatu tangu wayasilishe, ikiwa ni; Mizani ya kupima mifugo, Maji ya kunyweshea mifugo, machinjio, Josho, pamoja na  umeme.

“Tulihitaji maji hapa ili mifugo isije ikafa wakati inasubiri kuuzwa kwa kukosa maji, lakini umeme hapa ni muhimu kwani biashara zetu zinafanyika usiku, tayari hadi jenereta imeletwa kwa ajili ya kuhakikisha biashara haikwami kwa dharura yoyote ile, lakini mizani itasaidia kutowauza mifugo kwa kuangalia kwa macho bali kwa uzito wao” alisema Laizer

Mhagama alitoa maagizo hayo baada ya kukagua  Soko la kimkakati lililojengwa na Serikali kupitia Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Soko hilo litawanufaisha wananchi wapatao 14,2000  wa wilayani Longido ambapo asilimia 95 ni wafugaji na wanaojishughulisha na biashara za mifugo.

Soko  hilo la kimkakati ambalo halijafunguliwa rasmi , tayari halmashauri ya wilaya hiyo imeweza kukusanya mapato ya kiasi cha shilingi milioni 106 kwa mwaka  2016/2017 ambapo kwa makusanyo hayo yamewezesha halmashauri hiyo kuvunja rekodi ya miaka kumi iliyopita kwa kukusanya shilingi bilioni 1.3 kwa mara ya kwanza  kwani awali mapato yake yalikuwa chini ya bilioni moja.

MIVARF;  ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini  iliyobuniwa  na serikali ya Tanzania  kwa  kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).   Programu hii inatekelezwa  katika mikoa 29 ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani  tangu mwaka 2011.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: