Meneja wa kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar Abdallah Suleiman Ally akiongea na waandishi wa habari leo Zanzibar wakati akitangaza kuanza kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria.
Meneja Miradi kutoka VectorWorks akiongea na waandishi wa habari leo Zanzibar wakati akitangaza kuanza kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu

Wizara ya afya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria katika juhudi zake za kupambana na ugonjwa wa Malaria kinakusudia kutoa vyandarua laki moja na 95 elfu kwa mama wajawazito na watoto waliochini ya miaka mitano nchi nzima .

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar juu ya uzinduzi wa Kampeni ya kubwa ya matumizi ya vyandarua ambayo inatarajiwa kufanyika April nne mwaka huu visiwani Zanzibar Meneja wa utaribu wa kazi za kumaliza Malaria Zanzibar Abdallah Suleiman Ali amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimokatika mchakato wa kumaliza Malaria ambapo kwa sasa ni zaidi ya miaka kumi Zanzibar imekuwa ikipambana na ugonjwa huo .

Amesema Zanzibar kila kipindi kinachomaliza mvua za masika kumekuwa na kiwango kikubwa ugonjwa Malaria lakini jitihada mbali mbali zinachukuliwa ikiwemo kupiga dawa majumbani, kuhakikisha dawa zinapatikana katika vituo vya afya, na kuwepo kwa vipimo cha kuchunguzia ugonjwa huo na matumizi ya vyandarua vilivyopigwa dawa.

Amesema vyandarua ndio kinga tahabiti ya kujikinga na Malaria ambapo kwa Zanzibar Asilimia 77 ya Wananchi wanatumia vyandarua kiwango ambacho bado hakijaridhisha kufikia vigenzo vya wizara ya afya zanizbar ya Asilimia 100 na shirika la afya ulimwenguni WHO Asilimia 85.

Hata hivyo Meneja Abdallah amesema kwa sasa licha ya Zanzibar kupunguza maambuzi ya wagonjwa wa Malaria lakini amekiri ugonjwa huo bado upo chini ya Asilimia moja na ambapo vigezo vinavyotumika kuhakikisha Wananchi wanaobainika kuwa na vimelea anafuatiliwa katika familia yake ili kuhakikisha anakuwa salama dhidi ya ugonjwa huo.

Aidha amesema bado kuna maeneo ambayo yanatoka wagonjwa wengi wanaobainika kuwa na vimelea vya Malaria ikiwemo Wilaya ya Maghariba A na B , Wilaya ya kati na Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba na kwa wale Wananchi ambao wanatoka Tanzania bara katika mikoa ya Mwanza na Geita.

Kwa upande wake Waziri Nyoni Meneja Miradi wa VectorWorks amesema watakuwa na kazi ya kuhamasisha Jamii kuhakikisha vyandarua wanavyopatiwa wanavitumia ipasavyo ili kujikinga na ugonjwa na Malaria.

Kampeini ya kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria na kuratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria Zanzibar - ZAMEP .


Share To:

msumbanews

Post A Comment: