Waziri wa kilimo na ushirika Dkt. Charles Tizeba amepokea ripoti ya uchunguzi wa sakata la korosho zilizokutwa na mawe nchini Vietnam kisha kumuagiza katibu mkuu wizara hiyo kushirikiana na vyombo vya dola kuwakamata na kuwahoji wote waliohusika.
Dkt. Tizeba ametoa agizo hilo mjini Dodoma baada ya kupokea ripoti ya timu ya uchunguzi aliyounda Februari mwaka huu kutoka kwa makamu mwenyekiti wa timu hiyo Kassim Mbufu, ili kuchunguza sakata hilo ambalo limewataja baadhi ya maafisa wa serikali waliosimamia mchakato mzima wa kusafirisha korosho hizo kuanzia bandari ya Mtwara, Dar es salaam hadi Vietnam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti makamu mwenyekiti timu hiyo Kassim Mbufu ameshauri serikali kufanya mazungumzo na serikali ya Vietnam na kuwaeleza hatua walizochukua ili kuzuia udanganyifu huo.
Kwa upande mwingine, Waziri Tizeba ameahidi kufanya mazungumzo na wabunge wa Vietnam wanaotarajiwa kuwasilli nchini hivi karibuni kwa niaba ya serikali ya nchi yao ili kuwaeleza hatua walizochukua na jinsi ya kuzuia vitendo hivyo vyenye lengo la kuharibu soko la korosho ya Tanzania.
Post A Comment: