WATU watano wamenusurika kifo baada ya nyumba kuteketea kwa moto, katika kitongoji cha Kidongo Chekundu kata ya Magomeni wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Hili ni tukio la pili linalohusiana na janga la moto kutokea ndani ya wiki moja mkoani hapo ambapo machi 11 ,nyumba ya Makulata Petro iliungua huko Magwila wilaya ya Chalinze na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi wawili .

Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna alielezea tukio hilo ,limetokea machi 18 saa 5:30 asubuhi .

Alisema ,moto huo umeteketeza nyumba hiyo na kwasasa majeruhi hao wanapatiwa matibabu hospitali ya wilaya ya Bagamoyo .

Kamanda Shanna aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Emmanuel Nangu(33) mfanyabiashara ambae ameungua miguu na mke wake Victoria Mushi (32) aliyejeruhiwa kifuani na mikononi .

Mwingine ni msichana wa kazi Jovina Mapinduzi (16) aliyeungua miguuni na mapaja.


Aidha kamanda huyo alisema ,moto huo ulipotokea mitungi miwili ya gesi ilipasuka na kuruka juu na kupasua paa kisha kutoka nje na kuwajeruhi pia wapita njia ambao ni Msafiri Mohammed (36) na Hadija Juma (22) ambaye anuvunjika mguu.

"Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na kinachunguzwa licha ya kuwa na dhana mbili juu ya moto huo moja ni mitungi ya gesi na tatizo la umeme," alisema Shanna.

Alieleza wananchi wanapaswa kuangalia miundombinu ya umeme kwani baadhi ya nyumba ni michakavu.

"Kikosi cha zimamoto kinapaswa kutoa elimu kwa wananchi ili kutambua mitungi ya gesi ambayo haina matatizo " alifafanua kamanda Shanna.

Kamanda Shanna alisema, shirika la umeme (Tanesco) linapaswa kutoa elimu kwa jamii juu ya kufanya marekebisho ya miundombinu ya umeme kwenye nyumba zao.

Aliwaasa wenye nyumba kutoa elimu kwa wadada na wakaka wanaowaweka kufanya kazi kwenye nyumba zao ,ili kujua matumizi ya gesi na vyombo vya umeme.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: