Rapa Roma Mkatoliki ambaye mpaka sasa anatamba na wimbo wake 'Zimbabwe' amekuwa miongoni mwa watu walionesha hisia zao za kuguswa na maisha wanayopitia wanawake katika nyanja zote na kudai anawaonea huruma sana japokuwa anawapenda kupita maelezo.
Roma amebainisha hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii ikiwa kama ishara ya kuonesha mapenzi yake aliyokuwa nayo katika kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo huwa inaadhimishwa kila ifikapo Marchi 8 ya kila mwaka ulimwenguni kote.
"Namuonea huruma mama anayezaa kwa mshono na hata anayesukuma huku daktari kaweka mgomo, wengi wanaishi kama watumwa au chombo cha starehe ya ngono. Je kipi kinawea kukuuma mwanaume 'buzi' aliyechunwa au kahaba aliyenyimwa mtonyo. Nawapenda sana dada zangu pamoja na wanawake wote", amesema Roma.
Kwa upande mwingine, Roma amewafumbua macho wanaume wenzake kwa namna moja ama nyingine kwa kuwaambia wawe makini na wanawake kutokana na wao kuwa chombe chenye thamani kubwa duniani na kuwataka wavitunze imara.
Post A Comment: