MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,ameweka wazi kuwa vituo vya afya katika jimbo hilo vinakabiliwana na ukosefu wa vyumba vya kuhifadhia maiti .
Amesema changamoto hiyo ni kubwa ambapo husababisha wananchi kupeleka maiti za ndugu zao kwenye Hospitali teule ya rufaa ya Tumbi na wilaya ya Bagamoyo ambako kuna mbali mrefu.
Aliyasema hayo mjini Chalinze,wakati akizungumza na baadhi ya wananchi,na kusema shida kubwa inatokea hasa pale mgonjwa anapokuwa amefariki.
Ridhiwani alisema jimbo zima la Chalinze hakuna chumba cha kuhifadhia maiti kwenye vituo vyote vya afya hali ambayo imekuwa mtihani mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo .
"Hali ni mbaya kwa wenzetu wa kata ya Kibindu ambao wanapeleka maiti Hospitali ya Bwagala wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ,”
"Wananchi wanaingia gharama kwenda kuhifadhi maiti sehemu nyingine ambako ni mbali na maeneo yao"
“Tunaishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya afya pamoja na zahanati lakini changamoto yetu kubwa ni ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti ambapo tunajitahidi kufanya njia ili kuhakikisha tunajenga chumba hicho,” alisema Ridhiwani.

Post A Comment: