Mgogoro wa ardhi kati ya pori tengefu la mkungunero hifadhi ya Tarangire na wakazi wa kijiji cha kimotorok wilaya ya simanjiro umechukua sura mpya baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa manyara kufika katika eneo ilo na kutoa siku kumi kwa wataalam wa ardhi kuhakiki upya alama za mipaka.
Baada ya kufika katika eneo ilo kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Manyara ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Manyara Alaxander Mnyeti ilikagua mipaka na kupata maelezo kutoka kwa wananchi kisha ikatoa agizo ilo la kuwataka wananchi kutokundoka katika eneo mpaka uhakiki wa mipaka utakapofanyika upya kutoka idara ya ardhi ambalo katibu tawala msaidizi mundombinu wa mkoa huo bi suma tukampele mwakasitu anaahidi kuyatekeleza kwa umakini mkubwa maagizo hayo.
kwa upande wao wakazi wa kijiji cha kimotorok walipata nafasi ya kutoa madukuduku yao mbele ya Mkuu wa mkoa wa Manyara wanasema hawawezi kuondoka katika eneo kwani wamekaa tangu mwaka sabini na mbili na mipaka ya hifadhi ya tarangire wanaijua lakini wanshangaa kwanii wameongeza mipaka hyo huku Mbunge wa simanjiro James ole Milya akiwataka wataalamu hao kufanya uhakiki bila kupendelea upande wowote.
Post A Comment: