Jopo la Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Maafisa Ustawi wa Jamii, Wanasheria pamoja na Askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuwa wamejidhatiti vyema kuwasikiliza kinamama waliotelekezwa na hawapatiwi pesa ya matunzo ya mtoto kwenye zoezi la siku tano za kuwapatia msaada wa kisheria kinamama hao linalotaraji kuanza April 09 Mwaka huu.
Akizungumza na wataalamu hao Makonda amesema tatizo la wamama waliotelekezwa ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya tabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto wenye chuki na Baba zao.
Makonda amesema lengo la Zoezi hilo sio ugomvi bali ni kumwezesha Mtoto kupata mahitaji ili aweze kuitumia vyema fursa ya elimu bure chini ya serikali ya awamu ya tano.
Aidha Makonda amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha wanawasikiliza kinamama kwa umakini na kusimamia haki pasipo upendeleo.
Pamoja na hayo Makonda amesema wapo kinababa ambao wameanza kutoa fedha ya matunzo ya Mtoto baana ya kusikia tangazo ambapo amewasihi kinamama hao kufika April 09 kwaajili ya kuonana na wataalamu ili waweke makubaliano kwenye mfumo rasmi wa kimaandishi.
IFIKE HATUA MWANAUME UKIMPA MWANAMKE UJAUZITO BILA MPANGILIO AOGOPE KAMA ILIVYO KWENYE UBAKAJI

Post A Comment: