Machozi ya furaha jana yameitoka familia ya kijana Ahmed Albaity baada ya kukamilika kwa Safari ya matibabu kwa kijana wao kuelekea Nchini China safari iliyofanikishwa kwa jitiada binafsi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambae amejitolea kugharamia fedha ya Usafiri, Matibabu na Malazi kwa kijana huyo na hatimae jioni ya leo RC Makonda amemsindikiza Ahmed Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa safari.
Ahmed alipangiwa na Madaktari kwenda kupatiwa Matibabu China tokea Miaka miwili iliyopita lakini hakuweza kwenda kutokana na kushindwa kumudu gharama lakini kupitia jitiada binafsi za RC Makonda amefanikisha Safari ya Matibabu kwa Ahmed.
Ahmed Albaity amesafiri jioni ya leo akiongozana na wasaidizi Watatu ambapo RC Makonda amewafanikishia kupata fedha ya Tickets Nne za Ndege (first class), fedha ya matibabu na fedha ya kujikimu ambapo kwa ujumla ni zaidi ya Million 107.
RC Makonda amesema ataendelea kumsaidia Ahmed kwa kadiri ya uwezo wake ili aweze kurudi katika Hali yake ya kawaida ambapo amewashukuru wadau wote waliomchangia hadi kufanikisha safari hiyo.
"Nafasi ya Ukuu wa Mkoa sio yangu bali ni ya watu na watu wana changamoto zao hivyo tunalazimika kutoka kwenda kuona mahitaji ya wananchi na hatimae waone thamani ya uongozi na Serikali yao, hatuna bajeti lakini Mimi kama Makonda niliniliona vyema niwatafute Marafiki zangu ili tumsaidie ndugu yetu Ahmed apate matibabu na kurejesha tabasamu, ninayo furaha kusema tumefanikiwa kupata Dola 52,000 sawa na zaidi ya Million 107" Alisema RC Makonda.
RC Makonda amewasihi wananchi kuwa na Moyo wa kusaidiana kwenye matatizo na kuombeana heri.
Kwa upande wake Ahmed amemshukuru Rais Dr. John Magufuli kwa kumteua RC Makonda kuongoza Mkoa wa Dar es salaam ambapo kupitia yeye amefanikisha ndoto yake ya kupatiwa matibabu Nje ya Nchi.
Aidha amesema wana Dar es salaam wanapaswa kujivunia kupata bahati ya kipekee ya kuwa na kiongozi imara anaejali wananchi wake pasipokujali Dini wala kabila.
HUU NDIO UONGOZI UNAOACHA ALAMA.
Post A Comment: