Mifuko hiyo 2,400 ina uwezo wa kufyatua Tofali 70,000 ambazo zitejenga ofisi 14 za kisasa kwaajili ya Walimu.
Akipokea mifuko hiyo Makonda amesema shughuli ya ujenzi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri ambapo amewashukuru wadau wote wanaoendelea kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi na mwisho wa siku tuwe na wataalamu wa kutosha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Dar es salaam Bwana Tumaini Wilfred amesema wameguswa Sana na jitiada zinazofanywa na RC Makonda kwenye kuboresha mazingira ya walimu ndio maana wameona na hao Kama ushirika wasibaki Nyuma jambo hilo jema linalolenga kuleta ukombozi wa fikra.
Aidha Bwana Tumaini amesema Ushirika utaendelea kuunga mkono kwa kila hali juhudi zinazifanywa na Makonda.
Post A Comment: