Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanakuwa na wataalamu wa mahesabu katika biashara zao pamoja na kutoka risiti kila wanapofanya mauzo ili kuondokana changamoto ya kukadiriwa ulipaji wa kodi kobwa isiyoendana na uhalisia wa mauzo yao.
Gambo amesema hayo Leo wakati akizindua wiki ya elimu kwa mlipa kodi Mkoa wa Arusha ambapo ameeleza kuwa wafanya biashara wakiwa na wataalamu hao wataweza kuwasaidia kuaandaa taarifa ya mauzo vizuri itayoonyesha uhalisia wa kodi wayopaswa kulipa pamoja na kuondokana na ulipaji wa faini kwa kukiuka sheria ya malaka kwa kutotoa risiti.
Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Faustine Mdesa ameeleza kuwa mamlaka hiyo inamkakati wa kuboresha utoaji wa elimu kwa mlipa kodi ambapo zoezi hilo litakuwa linafanyika kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kutoka nafasi ya elimu kwa upana zaidi.
Aidha katika uzinduzi huo baadhi wa wafanyabiashara kutoka katika kundi la mabroka wa madini na wamiliki wa migahawa wametoa changamoto zinazowakabili katika zoezi mzima za ulipaji wa kodi ambapo wameiomba mamlaka hiyo kuweka utaratibu mzuri utakaokuwa na tija kwako na kwa serikali.
Post A Comment: