Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh: Mrisho Mashaka Gambo akiwa ameambatana na Katibu hamasa wa Vijana Ndg.Omary Lumato pamoja na Diwani wa Kata ya Ngarenaro Ndg.Isaya Doitha.
Diwani wa kata Ngarenaro Ndg.Isaya Doitha Akimpa maelekezo  na Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo kuhusu hadha wanazopata wakazi wa mtaa wa Kambi ya Fisi.
Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo akiwa ameambatana na Katibu Hamasa wa Uvccm Mkoa Ndg. Omary Lumato.
Diwani Doitha Akimuonyesha Mkuu wa Mkoa Madhara yaliyotokana na mfereji unaoteremsha maji kwenye makazi ya watu.
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Arusha Eng. Johnny Kalupale akiwa amefuatiwa na Katibu Hamasa Uvccm Mkoa Ndg. Omary Lumato wakimsikiliza Mkuu wa mkoa kwa makini.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh: Mrisho Mashaka Gambo leo akiwa ameambatana na meneja wa Tanroads pamoja na Diwani wa Ngarenaro wametembela na kuona madhara ya mfereji unaoteremsha maji kwenye makazi ya watu katika kata ya Ngarenaro Mtaa wa Kambi ya Fisi.

Akizungumza na Wakazi wa eneo hilo baada ya kuona madhara yaliyosababishwa na mfereji huo Mh: Gambo waliwataka wakazibwa mtaa huonkuwa wapole katika kipindi hiki serikali zikifanya juhudi za kutatua tatizo hilo na sio kuingiaza siasa katika masuala ya kimaendeleo, na kumuagiza Meneja wa Tanroads Mkoa wa Arusha Eng. Johnny Kalupale kuhakikisha jambo hilo linapatiwa ufumbuzi kwa haraka.

Naye Meneja wa Tanroads amewataka wakazi wote ambao wamejenga pembezoni mwa mfereji huo kuwa ndani ya wiki mbili wataanza ukarabati wa mfereji huo
wawe tayari na kutoa ushirikiano katika kufanya ukarabati wa mfereji huo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: