Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, Dkt. Binilith Mahenge akiwasili Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma akiwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi Idara ya Uhamiaji mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, Dkt. Binilith Mahenge akitia saini katika Kitabu cha Wageni Ofisini kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Naibu Kamishna Peter Kundy alipofanya ziara ya kikazi Idara ya Uhamiaji kukagua utendaji kazi wa Idara hiyo mkoani kwake. Mkuu wa mkoa aliongozana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, Dkt. Binilith Mahenge akifuatilia taarifa ya utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma ilipokuwa ikisomwa na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Naibu Kamishna Peter Kundy wakati wa kikao cha pamoja baina yake na watendaji wa Idara hiyo mkoani mwake.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Kadenge akiongea na watendaji wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Dodoma wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa huo alipotembelea kukagua undajikazi kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani mwake.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na Maafisa na Askari wa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma katika Ukumbi wa Ofisi ya Afisa Uhamiaji Mkoa huo wakati wa ziara ya kikaziya kukagua utendaji kazi wa Idara hiyo mkoani kwake. Katika ziara hiyo Mkuu wa mkoa aliongozana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, Dkt. Binilith Mahenge akionesha ramani ya Kiwanja kinachotarajiwa kujengwa jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya Uhamiaji, kiwanja hicho chenye ujazo wa Mita za mraba 9775 kimetolewa na Serikali ya Mkoa ili kufanikisha ujenzi wa tarajiwa. Anayemuonesha ramani Mkuu wa Mkoa ni Naibu Kamishna Peter Kundy, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma.
Post A Comment: