Na Ferdinand Shayo,arusha.
Mratibu wa Chama cha Wafanyakazi Mkoa wa Arusha (TUCTA) Samweli Magero  amesema kuwa tayari maandalizi ya awali ya mei mosi kitaifa itakayofanyika mkoani arusha yako katika hatua ya awali ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Raisi  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Ameeleza kuwa maandalizi ya awali yameshafanyika kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa arusha ambapo wanatarajia kuwa sherehe hizo zitafanya vizuri na kuwa na tija kwa taifa.

Hivyo ametoa wito kwa Wafanyakazi na Wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla kushiriki katika sherehe hizo muhimu  kwa wafanyakazi.

“Kabla ya sherehe hizi kutakua na maonyesho ya OSHA yanayohusu usalama maeneo ya kazi hivyo nitoe rai kwa wakazi wa Arusha kushiriki vyema” Alisema Magero

Alisema kuwa Wakazi wa Arusha wanapaswa kushirki katika sherehe hizo kama mkoa ambao umechaguliwa kuwa mwenyeji wa shughuli hizo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: