Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho Machi
26, 2018 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kupokea magari 181 ambayo
yatakuwa yakitumika kusambaza madawa vijijini na mjini.
Taarifa
hiyo iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas imeweka
wazi kuwa Rais Magufuli ndiye atakuwa mgeni rasmi na kuzindua magari
hayo 181 yaliyopo chini ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
"Mageuzi
Sekta ya Afya yanaendelea, usikose hafla ya kupokea magari mapya 181
kufikisha dawa na vifaa tiba zaidi mijini na vijijini" alisema Dkt Abass
Post A Comment: