Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Kamishna wa TRA, Waziri wa Fedha na katibu mkuu kuenda kuishughulika Shirika la Mapato Tanzania (TRA) ili iweze kuacha tabia zake chafu za kuwaongezea raia kodi za mapato pindi wanapokwenda kupata huduma hizo.
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kabla ya kuweka jiwe la msingi wa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya 'Standard Gauge' katika eneo la Ihumwa, Dodoma ambapo awamu ya kwanza ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2017, katika maeneo ya PUGU, Jijini Dar es Salaam.
"Napenda kuwahimiza watanzania wote kuendelea kulipa kodi ili kutekeleza miradi ya maendeleo nchini pamoja na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.
"Pamekuwepo na mtindo mtu anapokwenda kununua bidhaa anapewa risiti ya bei ndogo badala ya risiti anayotakiwa kupewa. Mtoa risiti na mpokeaji wote kwa pamoja wanaibia serikali na hivyo wanasababisha kuchelewesha maendeleo ya kujenga reli, ninawaomba watanzania tuwe wazalendo", amesema Rais Magufuli.
Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "TRA muangalie kodi zenu mnazozitoza, inawezekana nyingine ni kubwa mno kuliko miradi wanayotekeleza wananchi badala ya kuwa motisha kwa walipa kodi inakuwa kero kwao na badala yake wanabuni njia ya kukwepa kulipa kodi.
"Kwa hiyo TRA mjipange vizuri maana Kuna watu TRA si watu wazuri, na saa nyingine wanapokwenda kule wanaipaka matope serikali kwa kusema hii ndio dhana ya hapa kazi tu kumbe wao wanafanyakazi ya kuiba taifa".
Kwa upande mwingine, Dkt. Magufuli ameitaka TRA kuendelea kutoa elimu ya mlipa mkodi kwa wananchi ili kuweza kuwapa uelewa wanachi na waweze kulipa kodi kwa heshima kwa taifa lake.
Post A Comment: