Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kuwapongeza Wizara ya Ujenzi na mkandarasi aliyefanikisha ujenzi wa barabra ya Uyovu- Bwanga na kudai kuwa watu wa CHADEMA watawahi kwa ajili ya maandamano.
Magufuli amesema hayo leo Machi 10, 2018 akiwa kwenye ufunguzi wa barabara Uyovu - Bwanga, Bukombe mkoani Geita na kusema kuwa serikali imefanya maendeleo kwa ujenzi wa barabara na kudai hayo ndiyo mambo ambayo yeye anayahitaji kwenye serikali yake, aidha Rais Magufuli amedai kuwa kuna watu hawafurahii maendeleo ya Tanzania ndiyo maana wamekuwa wakijitahidi kufanya chokochoko.
"Nani afurahi nchii hii inayokaa kwa amani nyinyi pale mmekaa yupo wa ACT Wazalendo na wa CHADEMA yupo pale amekaa sawasawa kila mtu na kila mahali wote tunajiona ndugu kwa sababu maendeleo hayana chama. Tunajenga Hospitali ile huyu wa ACT atashindwa kwenda pale? Barabara hii wa CHADEMA si ndiyo wanawahi kwenda kuandamana mle hayo ndio maendeleo ninayotaka ya nchi yangu, hayo ndiyo maendeleo ya Watanzania na ndiyo maana nawapongeza sana Wizara ya ujenzi kwa kumaliza hii barabara" alisema Rais Magufuli
Post A Comment: