Generali Kale Kayihura.
RAIS  Yoweri Museveni wa Uganda ametengua uteuzi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo IGP Generali Kale Kayihura na Waziri wa Usalama Generali Henry Tumukunde mara moja.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya nchi hiyo leo imesema kwamba Rais Yoweri Museveni amemteuwa Okoth Ochola ambaye alikuwa Naibu Mkuu wa jeshi la Polisi  kuwa  mkuu mpya wa jeshi hilo la Polisi IGP. Taarifa hiyo pia inasema Rais Museveni amemteuwa Geberali Elly Tumwine, kuwa Waziri mpya wa usalama akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Geberali Tumukunde.

Aidha, Brigadia Sabiiti Muzeei ameteuliwa kuwa naibu mkuu wa jeshi la polisi nchini humo DIGP. Rais Meseveni mnamo mwezi Mei 2 alimteuwa tena Geberali Kayihura kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa miaka mingine mitatu ambapi uteuzi huo haujatifikia hata mwaka mmoja.

Generali Kayihura, ambaye ni miongoni mwa washirika waliomsaidia rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, alikuwa ni afisa mwenye nguvu zaidi katika jeshi hilo la Uganda. Licha ya nguvu hiyo aliyonayo mara kwa mara amejikuta kwenye shinikizo na lawama ya kudaiwa kushindwa kukabiliana na matukio ya uhalifu na kulinda usalama wa watu na mali zao nchini humo.
Okoth Ochola aliyeteuliwa.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni imedaiwa kuwa zaidi ya wanawake 20 wameshauawa katika matukio vya mauaji tofauti katika maeneo ya Kampala huku sababu na suluhu haijapatikana. Mbali na wanawake hao pia nchi hiyo imekubwa na vifo vya raia wa kigeni watatu vilivyotokea mfululizo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Kupitia ujumbe katika ukurusa wake wa Twitter Rais Museveni, amesema: “Kwa Mamlaka niliyopewa kikatiba, nimemteua Jenerali Elly Tumwiine kuwa waziri wa usalama. Nimemteua pia bwana Okoth Ochola kama Mkuu wa Jeshi la Polisi. Naibu wake atakuwa ni Brigedia Sabiiti Muzeei.”

Mkuu huyo wa Polisi aliyeteguliwa aliteuliwa kushika wadhifa huo Mei 2017, ambapo Rais Museveni alimteua kuwa mkuu wa polisi kwa kipindi kingine cha miaka mitatu iliyokuwa ifikie tamati mwaka 2020, uteuzi uliozua malalamiko mengi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: