Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) 
Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020. 
"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020
Share To:

msumbanews

Post A Comment: